Ligi ya mabingwa Ulaya kuendelea tena

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Kombe la UEFA Champions

Michuano ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya inatarajiwa kuendelea tena kesho Jumanne kwa michezo kadhaa katika mechi za makundi.

Miongoni mwa mechi zitakazopigwa ni pamoja na mechi ya BATE Borislov dhidi ya Bayer Leverkusen.

Barcelona watachuana na AS Roma, Arsenal ikiikabili Dinamo Zagreb, Bayern Munich wakiivaa Olympiakos.

FC Porto dhidi ya Dynamo Kiev, na Maccabi Tel Aviv ya Israel ikicheza na Chelsea.