CECAFA: Malawi yaichapa Sudan

Image caption Kombe la CECAFA

Michuano ya CECAFA inaendelea kushika kasi huko Ethiopia, huku Malawi ikiifunga Sudan 2-1 kwenye mechi iliyochezwa jana.

Hapo jana pia timu ya Sudan Kusini iliichapa Djibouti 2-0.

Leo Jumanne, Zanzibar Heroes watacheza na Uganda ambao walichapwa 2-0 na Kenya zikiwa ni mechi za Kundi B, Tanzania Bara yaani Kilimanjaro Stars nao watavaana na Rwanda.