Barca wazima AS Roma, Arsenal wang'aa

Haki miliki ya picha AP
Image caption Suarez akisherehekea kufunga bao dhidi ya AS Roma

Barcelona wakiwa nyumbani wamechomoza na ushindi wa mabao 6-1 dhidi ya AS Roma katika mechi ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.

Bayern Munich wakiichapa Olympiakos mabao 4-0, Maccabi Tel Aviv wakilala hoi kwa Chelsea kwa kichapo cha mabao 4-0.

Arsenal walijiwekea hai matumaini ya kufuzu kwa hatua ya makundi kwa ushindi wa 3-0 dhidi ya Dinamo Zagreb.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Wachezaji wa Arsenal walalamika eneo la hatari la Dinamo Zagreb uwanjani Emirates.

BATE Borisov wakifungana bao 1-1 na Bayer Laverkusen, FC Porto wakilala 2-0 dhidi ya Dynamo Kiev, Zenit St P wakiichapa Valencia 2–0 na Lyon wakilala mbele ya KAA Gent bao 2-1.

Michuano hiyo inatarajia kuendelea tena hii leo kwa michezo kadhaa.

Miongoni mwa mechi hizo ni Man United dhdi ya PSV Eindhoven, Atletico Madrid na Galatasaray, Juventus dhidi ya Man City na Shakhtar Donetsk watawaalika Real Madrid.

Matokeo kamili ya mechi zilizochezwa ni kama ifuatavyo:

  • Barcelona 6 - 1 AS Roma
  • Arsenal 3 - 0 Dinamo Zagreb
  • Bayern Munich 4 - 0 Olympiakos
  • Maccabi Tel-Aviv 0 - 4 Chelsea
  • BATE Borisov 1 - 1 Bayer Leverkusen
  • FC Porto 0 - 2 Dynamo Kiev
  • Zenit St Petersburg 2 - 0 Valencia
  • Lyon 1 - 2 KAA Gent