Andy Murray tayari kwa Davis Cup

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Kikosi cha Timu ya Tennis ya Uingereza

Timu ya Taifa ya Uingereza ya Tenisi, imewasili nchini Ubegiji kwa mchezo wa fainali ya Davis Cup utakaopigwa ijumaa nchini humo.

Timu hiyo inaongozwa na Andy Murray imewasili chini ya uangalizi wa ulinzi mkubwa kufuatia tishio la matukio ya kigaidi ambayo yameonekana kutishia amani nchini ubelgiji.

Timu hiyo inayojulikana pia kama Great britain ilipaswa kufika nchini humo tangu Jumapili lakini ikaahirisha kutokana na masuala ya kiusalama zaidi.

Kikosi cha Uingereza kinawakilishwa na Andy Murray, Jamie, Kyle Edmund, Dominic Inglot na James Ward ambao tayari wapo nchini Ubelgiji.