Djibouti na Zanzibar Heroes hali tete

Image caption Zanzibar Heroes

Michuano ya CECAFA CHALENJI CUP 2015 imeendelea jana Jumatano kwa michezo minne ya hatua ya makundi.

Harambe stars ya kenya ilitoka sare ya bao 1-1 na Burundi, wenyeji Ethiopia wameifunga somalia bao 2-0, Malawi imeifunga Djibouti bao bao 3-0.

Sudani Kusini ikitoshana nguvu na ndugu zao Sudan baada ya kutoka bila ya kufungana.

Michuano hiyo itaendelea tena kesho ijumaa kwa michezo kadhaa, Rwanda wataikabili somalia, vibonde Zanzibar Heroes watakuwa viwanjani dhidi ya Kenya.

Sudan Kusini watawakabili Malawi na Djibouti itachuana na Sudan.