Liverpool yaiadhibu Bordeaux-Europa Ligi

Haki miliki ya picha bbc
Image caption Kikosi cha Liverpool

Michuano ya Europa Ligi imeendelea tena jana kwa michezo mbalimbali katika hatua ya mtoano.

Miongoni mwa mechi zilizochezwa ni Liverpool dhidi ya Bordeaux ambapo Liverpool imechomoza na ushindi wa bao 2-1 mabao ambayo yamefungwa na James Milner pamoja na Christian Benteke.

Tottenham imeichapa Qarabag bao 1-0, Schalke 04 imeifunga Apoel Nicocia bao 1 – 0 , Monaco imechapwa bao 2-0 na Anderlecht.

FC Augsburg imelala bao 3-2 dhidi ya Athletic Bilbao, Ajax imeifunga Celtic bao 2-1 na FK Krasnodar imeiadhibu Borussia Dortmond bao 1-0.

Michuano hiyo itaendelea tena December 10 kwa michezo kadhaa, ikiwemo Fenerbahçe itaikabili Celtic, Tottenham watakuwa wenyeji wa Monaco, FC Sion itaikaribisha Liverpool.