Man City kuikabili Southampton

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Man City

Ligi kuu ya England inatarajiwa kuendelea tena kesho Jumamosi ambapo Aston Villa watawaalika Watford.

Bournemouth itaikabili Everton, Crystal Palace watakuwa wenyeji wa Newcastle, Man City watakuwa nyumbani Etihad dhidi ya Southampton.

Sunderland itachuana na Stoke City, nao Leicester city watakuwa wenyeji wa Manchester Utd.

Na Idhaa ya Kiswahili ya BBC itakutangazia moja kwa moja mechi kati ya Manchester City na Southampton kupitia matangazo ya Ulimwengu wa Soka.