Klitschko anataka marudio dhidi ya Fury

Haki miliki ya picha Getty

Bingwa wa uzani mzito wa dunia aliyeshindwa jana usiku Wladimir Klitschko sasa ameomba waandalizi wa ndondi ya uzani wa juu kumpa nafasi ya kuzichapa tena dhidi ya muingereza Tyson Fury mwakani .

Fury, 27, aliandikisha historia kwa kumchapa bingwa wa mataji yote matatu ya uzani wa juu kutoka Ukraine Klitschko kwa wingi wa pointi.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Klitschko anataka marudio dhidi ya Fury

Ushindi huo wa Fury sasa umetamatisha udhibiti wa miaka 9 wa raia huyo kutoka Ukraine wa ubingwa wa uzani wa juu katika ndondi za kulipwa.

Klitschko sasa ametaka kipengee cha mechi ya marudiano katika mkataba wa mechi hiyo utumike kuhakikisha ndiye anayepata fursa ya kwanza kuzichapa dhidi ya bondia huyo mcheshi kutoka Uingereza.

Haijabainika iwapo Uingereza ndiyo itakayoandaa mechi hiyo ya marudio au itaandaliwa nchini Ujerumani.

''japo nilipoteza ulingoni hapo jana ,ninaamini ninauwezo wa kuzichapa ,bado nina hamu ya kupigana''alisema Klitschko, 39.

''Bila shaka tutawatangazia lini na wapi tutapigana katika marudio ya ndondi za uzani wa juu'' aliongezea.

Bila kuchelea, Fuury alisema kuwa yuko tayari kupigana na bondia yeyote, ''Nataka kuwa bondia mashuhuri kwa hivyo niko tayari kupigana na mabondia wowote''

''Bila shaka itakuwapigano la kukata na shoka''

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Fury, aliibuka mshindi wa jumla ya pointi baada ya marefarii wote watatu kumpa pointi nyingi zaidi ya Klitschko.

Fury, aliibuka mshindi wa jumla ya pointi baada ya marefarii wote watatu kumpa pointi nyingi zaidi ya Klitschko.

Muingereza huyo alizoa alama 115-112, 115-112, 116-111 na hivyo kutawazwa bingwa wa dunia wa uzani wa juu wa taji la WBA, IBF na WBO.