Murray bingwa Davis Cup

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Uingereza imetwaa Kombe la Davis kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1936

Mcheza tenesi bora wa Uingereza Andy Murray amelipa taifa lake ubingwa wa michuano ya tenesi ya Davis Cup ya mchezaji mmoja mmoja.

Timu ya Uingereza imetwaa taji hilo kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1936 baada ya Murray kumshinda Mbelgiji David Goffin

Murray alimshinda mapinzani wake kwa jumla ya seti 6-3 7-5 6-3 na kumfanya Goffin kupoteza kwa jumla ya 3-1.

Nyota huyu wa tenesi amejiongezea historia baada ya kuwa ametwaa mataji ya michuano ya

Wimbledon, michuano ya wazi ya US Open na ile ya Michezo ya Olimpiki.