nusu fainali Cecafa :Uganda, Ethiopia

Image caption Kikosi cha Ethiopia

Timu ya Taifa ya Uganda na Wenyeji Ethiopia zimekua timu za kwanza kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya Cecafa 2015.

Wenyeji wa michuano hiyo Ethiopia wamesonga mbele kwa kuifunga timu Tanzania Kilimanjaro Stars kwa mikwaju ya penati Penati 4-3 baada ya suluhu ya 1-1 kwa Dakika 90.

Nayo timu ya Uganda The Cranes iliichapa Malawi 2-0 kwa mabao ya Farouq Miya na Ceaser Okuti, nahivyo kusonga mbele katika hatua ya nusu fainali.

Michezo ya nusu fainali ya pili itazikutanisha timu za Sudan Kusini dhidi ya ndugu zao Sudan, huku kenya wao wakipepeta na Rwanda