Chelsea kuboresha Stamford Bridge

Haki miliki ya picha PA
Image caption Iwapo uwanja utatanuliwa utakuwa na uwezo wa kubeba mashabiki 60,000

Klabu ya soka ya Chelsea imewasilisha maombi ya mpango wa kuupanua Uwanja wa Stamford Bridge ili kuweza kuingiza Mashabiki 60,000.

Maombi ya klabu hiyo yatachunguzwa na Manispaa ya London Borough of Hammersmith na Fulham ambayo pia imekaribisha maoni toka kwa Wananchi ambao watatakiwa kutoa ridhaa yao au pingamizi zao kabla ya Tarehe 8 Januari 2016.

Iwapo kutapitishwa kwa ujenzi huo majengo yaliyo jirani na uwanja huu yatalazimika kuvunjwaili kupisha ukarabati huo.

Chelsea, walianza kutumia uwanja wa Stamford Bridge, tangu 1905 ambapo mara ya mwisho kukarabatiwa na kupanuliwa ilikua ni katika Miaka ya 1990 na kuufanya uwe na uwezo wa kuchukua watazamaji 42,000.