Sudan, Rwanda zasonga mbele Cecafa

Image caption Rwanda yasonga mbele Cecafa

Timu mbili za Sudan na Rwanda zimefuzu kwa hatua ya nusu fainali ya michuano ya Cecafa baada ushindi katika michezo yao.

Sudani waliokua wakicheza na ndugu zao Sudan ya kusini walipata ushindi wa mabao 5-3 katika changamoto ya mikwaju ya penati baada ya kumaliza kwa sare ya 0-0 katika dakika 90 za mchezo.

Timu ya taifa ya Rwanda ikawaondoa mabingwa watetezi kenya kwa changamoto ya mikwaju ya penati kwa mabao 5-3, baada ya kushindwa kupata mshindi katika dakika 90 .

Michezo ya nusu fainali itafanyia siku ya alhamisi ambapo wenyeji Ethiopia itachuana na Uganda,huku Sudan ikipepetana na Rwanda.