Cahill asaini mkataba mpya Chelsea

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Gary Cahill

Beki wa kati wa timu ya taifa ya England na klabu ya Chelsea Gary Cahill amesaini mkataba mpya wa miaka minne na klabu yake.

Cahil ameichezea Chelsea jumla ya michezo 177 toka aliposajiliwa na miamba hao wa London mwaka 2012 akitokea timu ya Bolton, kwa dau la pauni milioni 7.

Mkataba wa sasa wa beki huyo kisiki ulikua umalizike mwishoni mwa msimu huu wa ligi, baada ya kusaini mkataba mpya Cahill alisema"Nimefanikiwa zaidi nikiwa hapa nitaendelea kujifunza, na kuisaidi timu yangu katika kutwaa mataji katika miaka minne ijayo,"

Msimu huu Cahil amecheza michezo 10 ya ligi kuu nchi England