Wenger: Huenda tukamkosa Carzola hadi Machi

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Carzola ameumia goti

Arsenal huenda ikamkosa kiungo wake wa kati Santi Cazorla hadi Machi mwaka ujao, meneja wao Arsene Wenger amefichua.

Mchezaji huyo wa miaka 30, anayechezea timu ya taifa ya Uhispania, aliumia goti wakati was are ya 1-1 ugenini Norwich Jumapili.

Klabu hiyo tayari inamkosa kiungo mwingine wa kati Francis Coquelin ambaye atakaa nje miezi mitatu baada ya kuumia kano za goti.

Hata hivyo, difenda Laurent Koscielny na mshambuliaji Theo Walcott wanaweza wakarejea kurudi dhidi ya Sunderland Jumapili.

Alexis Sanchez anauguza jeraha la misuli ya paja baada ya kuumia dhidi ya Norwich, huku Wenger akilazimika kutetea uamuzi wake wa kumchezesha mechi hiyo ya wikendi iliyopita.

“Mimi si mtaalamu, lakini mkitaka kunilaumu, ni sawa.”