Arsenal na Man Utd kuwa mawindoni Jumamosi

Arsenal Haki miliki ya picha bbc
Image caption Arsenal watakuwa nyumbani dhidi ya Sunderland

Mechi za Ligi ya Premia zitaendelea wikendi hii huku Arsenal, Manchester United na Chelsea wote wakishuka dimbani Jumamosi.

Arsenal watakuwa nyumbani Emirates dhidi ya Sunderland, Manchester United nao wakialika West Ham ugani Old Trafford.

Chelsea watajaribu bahati yao nyumbani Stamford Bridge dhidi ya vijana wapya ligi kuu Bournemouth.

Manchester City wanaoongoza jedwali na alama 29 watakuwa ugenini Stoke City huku Leicester wanaokwamilia nafasi ya pili na alama 29, lakini wakiwa wamepungukiwa na mabao, wakikaribishwa Swansea.

Man Utd ndiyo inayoshikilia nambari tatu na alama 28 ikifuatwa kwa karibu na Arsenal waliozoa alama 27.

Hii hapa ndiyo ratiba kamili ya mechi za wikendi hii:

Jumamosi 5 Desemba 2015

  • Stoke v Man City 12:45
  • Arsenal v Sunderland 15:00
  • Man Utd v West Ham 15:00
  • Southampton v Aston Villa 15:00
  • Swansea v Leicester 15:00
  • Watford v Norwich 15:00
  • West Brom v Tottenham 15:00
  • Chelsea v Bournemouth 17:30

Jumapili 6 Desemba 2015

  • Newcastle v Liverpool 16:00

Jumatatu 7 Dec 2015

  • Everton v Crystal Palace 20:00