‘Hamilton aliongozwa na hisia kuhamia Mercedes’

Lewis Haki miliki ya picha Getty
Image caption Lewis Hamilton amefanikiwa sana katika timu ya Mercedes

Mwendesha magari yaendayo kasi wa Timu ya Mercedes Lewis Hamilton amesema kuwa maamuzi ya Lewis Hamilton kuhamia Mercedes yaliongozwa na mvuto wa kihisia na si kutokana na umahiri wa timu hiyo, mwenzake wa zamani McLaren Jenson Button amesema.

Hamilton aliamua kuhamia Mercedes baada ya timu ya mashindano ya Singapore Grand Prix 2012, ambayo hakuweza kuyamaliza.

Hamilton ambaye aliwahi kushinda tuzo mbili kipindi cha awali, amekuwa akisisitiza mara nyingi maamuzi yake ya kuhamia Mercedes yalitokana na mipango ya magari hayo kwa ajili ya miaka ijayo, na kwamba alipata kupata ushauri kutoka kwa bosi wa timu yake Ross Brawn.

Lakini wakati ambapo Hamilton alifanya maamuzi hayo ya kuhamia Mercedes alikuwa mbali kwenye ushindani kuliko McLaren, ambao Hamilton alishindia mara nne.