Mshindi wa tuzo ya soka ya BBC Afrika kutangazwa

Tuzo
Image caption Wachezaji watano wanapigania kushinda tuzo hii

Mshindi wa Tuzo ya BBC ya mwanasoka bora wa Afrika wa mwaka 2015 atatangazwa leo jioni. Mwandishi wa BBC Peter Okwoche ndiye aliyeteuliwa kukabidhi tuzo hiyo kwa mshindi na ndiye mwenye bahasha yenye maelezo ya mshindi wa tuzo hiyo kwa mwaka huu.

Mshindi atatangazwa mwendo wa saa kumi na mbili unusu saa za Afrika Mashariki.

Watatu kati ya watano waliopenya katika mchujo, wanapigania kushinda kwa mara ya pili.

Kuna pia mshindi wa tuzo hiyo kwa mwaka uliopita raia wa Algeria Yacine Brahimi ambaye amefanya vizuri mwaka huu akiwa na klabu yake ya FC Porto.

Mwingine anayepigania kutwaa tuzo hiyo kwa mara ya pili ni mchezaji wa timu ya Swansea Andre Ayew, ambaye aliiwezesha timu ya Ghana kufanikiwa kutinga katika fainali za michuano ya kombe la mataifa ya Afrika.

Image caption Peter Okwoche

Mwingine ni Yaya Toure wa timu ya Manchester City na Ivory Coast, ambaye alitwaa ubingwa wa Afrika na Ivory Coast mapema mwaka huu.

Mwingine ambaye naye pia anatajwa kutwaa tuzo hiyo ni mshambuliaji wa timu za Gabon na Borussia Dortmund Pierre-Emerick Aubameyang, ambaye amekuwa akifumania nyavu tangu mwaka huu uanze.

Hata hivyo, msenegali Sadio Mane ambaye ameingia katika orodha ya mwisho kwa mara ya kwanza baada ya kufanya mambo makubwa akiwa na timu ya Southampton mwaka huu, mwaka mmoja alipofunga bao tatu katika ligi yenye ubavu wa haja na kasi uwapo uwanjani na kuandika historia.

Mshindi wa tuzo ya BBC ya Mwanasoka bora wa Afrika huamuliwa na mashabiki ambao hupiga kura.

Mshindi wa tuzo hiyo kwa mwaka huu atakabidhiwa rasmi tuzo katika hafla ambayp itaoneshwa moja kwa moja katika runinga ya BBC World TV, World Service radio na katika mitandao ya BBC.