Michuano ya Europa ligi yaendelea

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Rubin Kazan akiwa katika mshike mshike wa igi hiyo barani ulaya

Michuano ya Europa ligi imeendelea tena usiku wa jana kwa mechi kadhaa,Miongoni mwa mechi hizo ni Fenerbahçe ambayo imetoshana nguvu na celtic kufuatia sare ya bao 1 - 1, Tottenham imeiadhibu Monaco kwa ushindi wa bao 4 – 1,FC Sion imetoshana nguvu na Liverpool kwa sare ya kutofungana 0 – 0, Ajax imesare na Moldel kwa bao 1 – 1, Anderlecht imetakata kwa ushindi wa bao 2 – 1 dhidi ya FK Qarabag, Apoel Nicocia imechapwa bao 3-1 na Sparta Prague, huku Asteras Tripolis ikiadhibiwa bao 4-0 na Schalke 04, Ath Bilbao imetoshana nguvu na Z Alkmaar kwa 2-2, Augsbarg imeifunga P'zan Belgrade bao 3-1, Bordeaux imegawana pointi na Rubin Kazan naada ya kufungana bao 2 – 2 , Borrussia Dortmond imefungwa na Paok salonika bao 1-0 ,na FK Qabala imelala kwa bao 3-0 na FK Krasnodar.