Man Utd kushuka dimbani ugenini Bournemouth

Manchester United Haki miliki ya picha EPA
Image caption Manchester United wanashikilia nambari nne kwenye jedwali EPL

Ligi kuu ya soka ya England itaendelea wikendi hii, ikianza kwa mchezo wa mapema Jumamosi kati ya Norwich na Everton.

Crystal Palace watakuwa wenyeji wa Southampton, Man City watawaalika Swansea City, Sunderland watawakaribisha Watford, West Ham United itakuwa nyumbani dhidi ya Stoke city, na Bournemouth wataikabili Man United.

Mchezo kati ya Manchester City na Swansea City utatangazwa moja kwa moja na Idhaa ya Kiswahili ya BBC kupitia matangazo yake ya ulimwengu wa soka.

Na Jumapili ligi hiyo itaendelea tena kwa michezo mitatu ambapo Aston Villa watakuwa wenyeji dhidi ya Arsenal, Liverpool watakuwa nyumbani Anfield dhidi ya West Brom, na Tottenham watawaalika Newcastle United.

Ratiba kamili ndiyo hii hapa (Saa za Afrika Mashariki):

Jumamosi 12 Desemba 2015

  • Norwich v Everton 15:45
  • Crystal Palace v Southampton 18:00
  • Man City v Swansea 18:00
  • Sunderland v Watford 18:00
  • West Ham v Stoke 18:00
  • Bournemouth v Man Utd 20:30

Jumapili 13 Desemba 2015

  • Aston Villa v Arsenal 16:30
  • Liverpool v West Brom 19:00
  • Tottenham v Newcastle 19:00

Jumatatu 14 Desemba 2015

  • Leicester v Chelsea 23:00