Real Madrid, Arsenal na Bayern zang’ara

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Real Madrid

Michuano ya klabu bingwa ulaya Hatua ya makundi imehitimishwa jana usiku kwa michezo mbalimbali ambapo katika mechi za kundi D, Bayer Leverkusen imegawana pointi na Barcelona kufuatia sare ya bao 1–1, Olympiakos wakiwa nyumbani dhidi ya Arsenal wakaambulia kichapo cha mabao 3-0 ambayo yamefungwa na mchezaji Olivier Girioud ikiwa ni Hat-trick kwa mchezaji huyo.

Chelsea wakiwa nyumbani Stamford Bridge wao wametakata kwa ushindi wa mabao 2 – 0 dhidi ya FC Porto, Valencia imechapwa bao 2-0 na Lyon,

FC Roma imetoshana nguvu na BATE Borislov baada ya sare ya kutofungana 0-0, Bayern Munich imeichapa Dinamo Zagreb bao 2-0, Dynamo Kiev imewafunga Macabbi Tel-Aviv bao 1–0 na KAA Gent imeifunga Zenit bao 2–1 .

Kwa matokeo hayo sasa Timu za Real Madrid, Wolfsburg, Atletico Madrid, Man City, Barcelona, Bayern Munich, Chelsea na Zenit ndio timu ambazo zimeongoza katika makundi na kuungana na timu nyingine katika hatua ya 16 bora, na kuingia droo ya raundi ya muondoano ya timu 16 ambayo inatarajiwa kufanyika Desemba 14.

Matokeo kamili ya mechi za UEFA zilizochezwa Jumatano:

  • Bayer Leverkusen 1 - 1 Barcelona
  • Olympiakos 0 - 3 Arsenal
  • Chelsea 2 - 0 FC Porto
  • Valencia 0 - 2 Lyon
  • Roma 0 - 0 BATE Borisov
  • Dinamo Zagreb 0 - 2 Bayern Munich
  • Dynamo Kiev 1 - 0 M'bi Tel-Aviv
  • KAA Gent 2 - 1 Zenit St Petersburg