Van Gaal:Sina wasiwasi kuhusu wadhfa wangu

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Louis Van Gaal

Mkufunzi wa kilabu ya Manchester United Louis Van Gaal amesema kuwa hana wasiwasi kuhusu wadhfa wake na kwamba kikosi chake kinafaa kujaribu kushinda taji la Yuropa.

United iko katika nafasi ya nne katika ligi ya Uingereza ,ikiwa pointi tatu nyuma ya viongozi Leicester City,lakini imekosolewa kwa kushindwa kufunga mabao na kuonyesha mchezo mzuri msimu huu.

United lipoteza 3-2 kwa Wolfsburg siku ya jumanne na hivyobasi kubanduliwa katika kinyang'anyiro cha kilabu bingwa Ulaya.

''Nafanya bidii, ili kufanya tunachoweza kufanya'', alisema mkufunzi huyo wa umri wa miaka 64.

Na alipoulizwa iwapo alihisi wasiwasi wowote kuhusu wadhfa wake alijibu:Sina wasiwasi.Lazima ushinde na kushindwa katika michezo na hilo lazima likubalike.

''Tatizo ni kwamba lazima tukabiliane na matarajio,katika kilabu kama hii ni mengi mno''.