England kundi moja na Wales Euro 2016

Euro 2016 Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Michuano itaanza Juni 10

England wamewekwa kwenye kundi moja na Wales kwenye michuano ya taifa bingwa Ulaya itakayoandaliwa Ufaransa mwaka ujao.

Michuano hiyo itaanza kwa mechi ya ufunguzi dhidi ya wenyeji Ufaransa na Romania Juni 10.

Mechi kati ya Wales na England itachezwa Juni 16 mjini Lens.

Hafla ya kufanya droo hiyo imeongozwa na katibu mkuu wa Uefa Gianni Infantino.

Droo ya Euro 20116
Kundi A . Kundi B
1 Ufaransa 1 England
2 Romania 2 Urusi
3 Albania 3 Wales
4 Uswizi 4 Slovakia
Kundi C . Kundi D
1 Ujerumani 1 Uhispania
2 Ukraine 2 Jamhuri ya Czech
3 Poland 3 Uturuki
4 Ireland Kaskazini 4 Croatia
.
Kundi E Kundi F
1 Ubelgiji 1 Ureno
2 Italia 2 Iceland
3 Jamhuri ya Ireland 3 Austria
4 Sweden 4 Hungary