Manchester City warejea kileleni EPL

Yaya Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Toure alitawazwa mwanasoka bora wa BBC wa Afrika wa mwaka 2015 Ijumaa

Manchester City wamerejea kileleni mwa Ligi Kuu ya Uingereza baada ya kupata ushindi wa 2-1 dhidi ya Swansea City, wakipata bao kupitia mpira uliopigwa na Yaya Toure dakika za mwisho.

Dalili zote zilikuwa zimeonyesha kana kwambwa wangeondoka na ushindi wa 1-0 dhidi ya wageni wao, lakini Baf├ętimbi Gomis akasawazisha dakika za mwisho. Lakini mambo yalikuwa bado kwani kulikuwa bado na muda kwa Toure kugongesha mpira kwenye mgongo wa Kelechi Iheanacho, na mpira huo ukamkwepa Lukasz Fabianski na kuingia wavuni.

Bao la kwanza la City lilifungwa na Wilfried Bony.

Manchester City sasa wana alama 33 kileleni, wakifuatwa na Leicester City ambao watacheza mechi yao Jumatatu dhidi ya Chelsea.

Katika mechi nyingine za Jumamosi, Norwich walitoka sare ya 1-1 na Everton, Crystal Palace wakapata ushindi wa 1-0 dhidi ya Southampton, Watford nao wakiondoka kwa wageni wao Sunderland na alama tatu baada ya kushinda 1-0.

Upton Park, West Ham na Stoke City waliridhika na sare tasa.