Arsenal wapewa Barca ligi ya mabingwa Ulaya

AFC Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mabingwa watetezi Real Madrid watakutana na Roma

Arsenal ya Uingereza imepangwa na Barcelona ya Uhispania, ambao ndio mabingwa watetezi, kwenye hatua ya 16 bora Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.

Mechi hiyo itakuwa kama marudio ya fainali ya 2006, ambayo mabingwa hao wa Uhispania walishinda 2-1 kupitia mabao mawili ya dakika za mwisho mjini Paris.

Wenzao kutoka Uingereza Chelsea wamepewa miamba wa Ufaransa Paris Saint Germain baada ya droo kufanywa mjini Nyon, Uswisi. Hii itakuwa mara ya tatu mtawalia kwa Chelsea kukutana na PSG katika michuano ya Uefa.

Droo kamili:

  • Benfica (Ureno) v Zenit St Petersburg (Urusi)
  • Dynamo Kyiv (Ukraine) v Manchester City (Uingereza)
  • Juventus (Italia) v Bayern Munich (Ujerumani)
  • PSV (Uholanzi) v Atletico Madrid (Uhispania)
  • PSG (Ufaransa) v Chelsea (Uingereza)
  • Arsenal (Uingereza) v Barcelona (Uhispania)
  • Gent(Ubelgiji) v Wolfsburg(Ujerumani)
  • Roma (Italia) v Real Madrid (Uhispania)

Mechi za mkondo wa kwanza zimeratibiwa kucheza Februari 16-17 na 23-24. Mechi za marudiano ni Machi 8-9 na 15-16.