Man Utd kukabili Midtjylland Europa League

Man Utd Haki miliki ya picha PA
Image caption Man Utd waliondolewa Ligi ya Mabingwa baada ya kumaliza nambari tatu kundi lao

Manchester United watakutana na klabu ya Denmark Midtjylland katika hatua ya 32 bora baada ya kuondolewa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.

Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp naye atarejea Ujerumani kupeleka vijana wake wakabiliane na Augsburg.

Baada ya droo kufanywa, Tottenham Hotspur nao wamepewa vijana wa Serie A Fiorentina kwa mara ya pili mtawalia.

Valencia chini ya Gary Neville wamepewa Rapid Vienna.

Mechi za mkondo wa kwanza zitachezwa Februari 18 au 25 na marudiano Machi 10 na 17.

Klabu zote za Uingereza zitakuwa nyumbani mechi za marudiano.

Droo Kamili

Valencia v Rapid Vienna

Fiorentina v Tottenham Hotspur

Borussia Dortmund v FC Porto

Fenerbahce v Lokomotiv Moscow

Anderlecht v Olympiakos

Midtjylland v Manchester United

Augsburg v Liverpool

Sparta Prague v Krasnodar

Galatasaray v Lazio

Sion v Braga

Shakhtar Donetsk v Schalke

Marseille v Athletic Bilbao

Sevilla v Molde

Sporting Lisbon v Bayer Leverkusen

Villarreal v Napoli

Saint-Etienne v Basel