Leicester waadhibu Chelsea na kurudi kileleni

Chelsea Haki miliki ya picha Getty
Image caption Wachezaji wa Leicester City wakisherehekea ushindi dhidi ya Chelsea

Mabingwa watetezi wa ligi kuu England Chelsea wamezidi kutumbukia kwenye matatizo baada ya kupokezwa kichapo cha 2-1 na Leicester City.

Mshambuliaji wa Leicester Jamie Vardy ndie aliyeanza kupeleka msiba kwa The Blues baada ya kuandikisha bao la kwanza katika katika ya 34 ya mchezo. Winga Riyard Mahrez akaongeza bao la pili na la ushindi katika dakika ya 48 ya mchezo.

Bao pekee la kufutia machozi kwa upande wa Chelsea lilifungwa na Loic Remy aliyefunga kwa kichwa baada ya kupokea krosi nzuri kutoka kwa Pedro.

Kwa ushindi huu Leicester City wanarejea kileleni mwa ligi wakiwa na alama 35 baada ya kucheza michezo kumi na sita huku Chelsea wakijichimbia katika nafasi 16 wakiwa na alama 15 wakiwa wamepoteza michezo tisa katika michezo 16.

Mshambuliaji Jamei Vardy ameendelea kuongoza katika kinyang'anyiro cha mfungaji bora msimu huu akiwa sasa ametikisa nyavu mara 15 ligini msimu huu.