Yanga yapaa kileleni ligi ya Tanzania

Image caption Timu ya Yanga ya Tanzania

Timu ya soka ya Yanga imerejea tena kileleni mwa ligi ya Tanzania baada kupata ushindi dhidi ya African Sport.

Yanga wakicheza ugenini katika dimba Mkwakwani walipata ushindi wa bao 1-0 kwa bao liliwekwa kambani na kiungo Thabani Kamusoko.

Timu hiyo sasa inaongoza Ligi ikiwa na alama 27, na kuwazidi timu ya Azam FC kwa alama 1 huku Azam wakiwa na mchezo mmoja mkononi.

Ligi hiyo itaendelea tena kutimua vumbi mwishoni mwa wiki kwa michezo mbalimbali kuchezwa.