Barcelona fainali Kombe la dunia la Vilabu

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mshambuliaji wa Barcelona Luiz Suarez akipachika bao dhidi ya Guangzhou Evergrande. Barcelona ilishinda 3 -0 yote yakifungwa na Luiz Suarez

Mshambuliaji Luis Suarez ameipeleka timu yake ya Barcelona, katika hatua ya fainali ya kombe la dunia la vilabu.

Barcelona waliokua wakicheza dhidi ya Guangzhou Evergrande, walipata ushindi wa mabao 3-0 huku mshambuliaji nyota wa timu hiyo Luis Suarez akifunga mabao yote matatu.

Suarez alianza kuandika bao la kwanza katika dakika ya 39 kisha akaongeza la pili dakika ya 50 na kuhitisha kazi kwa bao la tatu kwa mkwaju wa penati katika dakika ya 67.

Barcelona watachuana na River Plate katika mchezo wa fainali itayofanyika desemba 20 katika uwanja wa Yokohama.