Chelsea, Man Utd kushuka dimbani EPL

Chelsea Haki miliki ya picha Getty
Image caption Chelsea watajaribu kufufua kampeni yao msimu huu dhidi ya Sunderland

Ligi Kuu ya Uingereza itarejelewa leo kwa mechi saba, Chelsea na Manchester United zikiwa miongoni mwa klabu zitakazocheza nyumbani.

Chelsea, walio alama moja pekee juu ya eneo la kushushwa daraja, watakuwa nyumbani kwa mechi ya kwanza bila meneja wao Jose Mourinho aliyefutwa Alhamisi.

Chelsea bado haijateua meneja mpya ingawa dalili zinaonyesha huenda Guus Hiddink akateuliwa kaimu meneja. Meneja huyo wa zamani wa Uholanzi aliwasili jana London kwa mazungumzo na maafisa wa klabu hiyo.

Chelsea wataongozwa na makocha wasaidizi Eddie Newton na Steve Holland.

Ratiba kamili ya mechi (Saa za Afrika Mashariki):

Jumamosi

  • Chelsea v Sunderland 18:00
  • Everton v Leicester 18:00
  • Man Utd v Norwich 18:00
  • Southampton v Tottenham 18:00
  • Stoke v Crystal Palace 18:00
  • West Brom v Bournemouth 18:00
  • Newcastle v Aston Villa 20:30

Jumapili

  • Watford v Liverpool 16:30
  • Swansea v West Ham 19:00

Jumatatu

  • Arsenal v Man City 23:00