Madrid yaiadhibu Rayo 10-2 La Liga.

Haki miliki ya picha AP

Klabu ya soka ya Real Madrid iliifanikiwa kuichapa Timu ya Rayo Vallecano Bao 10-2 katika Mechi ya ligi kuu ya ispania maarufu kama (La Liga ) .

Madrid walianza kufunga mabao kupitia Danilo na Rayo Vallecano wakasawazisha na kuongeza bao na kuongoza ikiwa ni bao 2-1.

Katika ushindi wa mabao hayo 10-2 -mbali na mchezaji Danilo mabao mengine ya madridi yalifungwa na wachezaji Gareth Bale mabao manne (4) , Cristiano Ronaldo mabao mawili (2), Karim Benzema mabao matatu (3), huku mabao ya Rayo Vallecano yakifungwa na Antonio Amaya Pamoja na Jozabed.

Ushindi huu umewabakisha Real Madrid katika Nafasi ya 3 wakiwa Pointi 2 nyuma ya Vinara Barcelona na Atletico Madrid .