Hiddink awataka wachezaji kuwa makini

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Guus Hiddink meneja mpya wa klabu ya Chelsea

Meneja mpya wa klabu ya Chelsea Guus Hiddink, amekitaka kikosi chake kuwa makini na kuzingatia uwepo wao katika timu hiyo.

Hiddink aliteuliwa wiki iliyopita kumbadili Jose Mourinho alietimuliwa na kupewa wadhifa huu hadi mwishoni mwa msimu huu.

Chelsea ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu England hadi sasa wapo Nafasi ya 15 baada ya kucheza Mechi 17.

amesema kimahesabu chelsea inawza kumaliza katika nafasi ya nne Msimu huu ili icheze Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya msimu ujao lakini ni kazi ngumu.

Hii ni mara ya pili kwa Hiddink kutua Chelsea mara ya kwanza ilikuwa Msimu wa 2008/09 alipotimuliwa Luiz Felipe Scolari na yeye kushika wadhifa wa Umeneja kwa Miezi Mitatu ya mwisho akiwasaidia Chelsea kutwaa FA CUP, kufika Nusu Fainali ya UEFA na kumaliza Nafasi ya tatu kwenye Ligi wakiwa na Pointi saba nyuma ya Manchester United.