Robin Soderling astaafu tenesi

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Robin Soderling

Aliyewahi kuwa mcheza Tenesi namba nne duniani Robin Soderling ameamua kustaafu rasmi mchezo huo baada ya kuugua homa ya tezi tangu mwaka 2011.

Robin mwenye miaka thelathini na mmoja ambaye ni rais wa Sweden,anasifika kwa kuwa mtu wa kwanza kuweza kumshinda Rafael Nadal katika michuano ya French Open mnamo mwaka 2009,na tangu wakati huo hakupata nafuu ya maradhi yake ili kurejea mchezoni.

Soderling alifanikiwa kuingia katika fainali za michuano hiyo ya French Open kwa miaka miwili mfululizo yaani 2009 na mwaka 2010,na ameweka bayana sababu za kustaafu kwake kwamba anatambua kuwa afya yake si nzuri kuweza kumruhusu kuendelea na mchezo wa tenesi katika ubora anaoutaka.

Na kwa sababu hiyo amechukua maamuzi ya kusitisha kipaji chake kama mchezaji wa kimataifa wa mchezo huo .

Robin pia katika historia yake amewahi kuingia katika robo fainali za mchezo huo katika viwanja vya Wimbledon na pia US Open,na mara zote alikuwa na matumaini ya kurejea viwanjani lakini hatimaye amekiri kushindwa.