Louis van Gaal awapasha waandishi.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Louis Van Gaal

Meneja wa Manchester United Louis van Gaal ambaye kwa sasa yuko katika hali mbaya ndani ya klabu hiyo kutokana na matokeo mabovu ya timu hiyo amezungumza kwa ukali dhidi ya waandishi wa habari kupitia Mahojiano na Wanahabari hao kuelekea mchezo wa Jumamosi na Timu ya Stoke City.

Kupitia mahojino hayo Van Gaal alisema najua mtaandika yote hayo,na kwa Sasa hatupo kwenye nafasi nzuri lakini kumbukeni Wiki nne zilizopita tulikuwa Namba moja kwenye Ligi na baada ya Wiki nne tunaweza kuwa wa Kwanza tena.

Mwisho Vaan Gaal aliwaambia Waandishi katika mkutano huo kuwa Nawatakia Krismasi njema na Mwaka Mpya mwema , na Furahieni Mvinyo na Mikate pamoja na Nyama ya Kusaga.