Carrick: Tunacheza kwa ajili ya Van Gaal

Man Utd Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Man Utd wameandikisha msururu wa matokeo mabaya

Nahodha msaidizi wa Manchester United, Michael Carrick amelalamika madai kuwa wachezaji wa klabu hiyo hawachezi vizuri ili kulinda kibarua cha kocha wao.

Wachezaji wa Man United wamelaumiwa baada ya kupoteza mchezo wa nne mfululizo dhidi ya Stoke City kwa kuchapwa mabao 2-0 Jumamosi.

Amesema: "Ni makosa kusema wachezaji hawajitumi kadri ya uwezo wao kwa ajili ya kocha Luis Van Gaal, inaumiza sana sisi sio watu wa aina hiyo."

Man United watashuka dimbani dhidi ya Chelsea katika mchezo Jumatatu jioni huku shinikizo kubwa likiwa kwa kocha wa kikosi hicho Lauis Van Gaal