EPL: Arsenal yapaa kileleni

Ozil Haki miliki ya picha Getty
Image caption Ozil alisaidia sana Arsenal mechi hiyo dhidi ya Bournemouth

Washika bunduki wa London, Arsenal wamekaa kileleni mwa ligi ya England kwa pointi 39 baada ya kuichapa Bournemouth kwa mabao 2-0.

Arsenal walipata mabao yao kupitia kwa beki Gabriel Paulista aliyefunga bao la kwanza dakika ya 27 ya mchezo kisha kiungo wa Ujerumani Mesut Ozil, akahitimisha kazi kwa bao la pili alilolifunga katika dakika ya 63.

Nao Mashetani Wekundu wa Man United walitoka sare ya 0-0 na mabingwa watetezi Chelsea, Everton wakicheza katika dimba lao la Goodson Park wakalala kwa kipigo cha mabao 4-3 kutoka kwa Stoke city.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Joselu alifungia Stoke City bao la tatu

Matokeo mengine ni:

  • Crystal Palace 0 – 0 Swansea
  • Norwich 2 – 0 Aston Villa
  • Watford 1 – 2 Tottenham
  • West Brom 1 – 0 Newcastle
  • West Ham 2 – 1 Southampton

Uongozi wa Arsenal huenda ukafikishwa kikomo leo iwapo Leicester City watafanikiwa kuandikisha ushindi dhidi ya miamba wa Etihad Manchester City kwenye mechi itakayochezwa baadaye leo.

Jedwali lilivyo kwa sasa:

Nambari Klabu Mechi Mabao Alama
1 Arsenal 19 15 39
2 Leicester 18 12 38
3 Tottenham 19 18 35
4 Man City 18 17 35
5 Crystal Palace 19 7 31
6 Man Utd 19 6 30
7 West Ham 19 5 29
8 Watford 19 4 29
9 Stoke 19 1 29
10 Liverpool 18 -1 27
11 Everton 19 7 26
12 Southampton 19 3 24
13 West Brom 19 -6 23
14 Chelsea 19 -6 20
15 Norwich 19 -10 20
16 Bournemouth 19 -12 20
17 Swansea 19 -8 19
18 Newcastle 19 -15 17
19 Sunderland 18 -18 12
20 Aston Villa 19 -19 8