Naismith kujiunga na Norwich City

Haki miliki ya picha All Sport
Image caption Steven Naismith

Mshambuliaji wa klabu ya Everton Steven Naismith anatarajiwa kujiunga na Norwich City mwezi Januari kwa dau la pauni milioni 8.

Naismith mwenye umri wa miaka 29 amecheza michezo mnne tu katika msimu huu wa ligi kuu England, lakini akiwa kafunga hat-trick kwenye mchezo dhidi ya Chelsea .

Mwanzo wa wiki mchezaji huyu alicheza kwa dakika 25 katika mchezo amabo Everton walilala kwa mabao 4-3 dhidi ya Stoke City.

Wakati wa dirisha kubwa la usajili la mwezi August Everton walikaa pau la pauni 7, Mshambuliaji huyu ameichezea timu yake jumla ya michezo 103 na kufunga magoli 18 toka aliposajiliwa kutoka Rangers ya Usikoch.