Moyes: Van Gaal anafaa apewe muda

Ma Utd Haki miliki ya picha EPA
Image caption Man Utd wameandikisha matokeo mabaya mechi za karibuni

Meneja wa zamani wa Manchester United David Moyes amesema klabu hiyo inafaa kumpa muda zaidi kocha wa sasa Louis van Gaal.

Timu hiyo kufanya vyema kwa kucheza michezo minane bila ushindi huku wakitolewa kwenye michuano Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.

Klabu hiyo pia imeshindwa kukaa katika nafasi nne za juu ligini.

"Nina imani wataendelea kushirikiana naye, anastahili kupata muda zaidi. Amewanunua wachezaji nyota na kwa kuzingatia niliyoyaona kule Uhispania, itachukua muda kwa wachezaji hawa kutoka nje kuzoea mchezo Uingereza. Kwa hivyo, nafikiri wanafaa kukwama naye," alisema meneja huyo wa zamani wa Man United.

Moyes amesema bodi ya Manchester United kawaida huwaunga mkono mameneja na anatumaini wataendelea kumuunga mkono.

Kwenye mahojiano na kipindi cha Clare Balding ya BT Sport, Moyes amesema wasimamizi wa Manchester United hawawezi kutaka klabu hiyo iwe ya kubadilisha badilisha mameneja ovyo ovyo.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Moyes alifutwa baada ya kuongoza Man Utd miezi 10

Van Gaal alichukua mikoba ya ukufunzi kutoka David Moyes Mei 2014 baada ya Moyes kutimuliwa baada ya klabu hiyo kufanya vibaya katika ligi kuu Uingereza na michuano ya bara Ulaya.

Moyes alikuwa ameongoza klabu hiyo kwa miezi 10 pekee baada ya kumrithi meneja wa muda mrefu Sir Alex Ferguson.

Baada ya kuondoka Old Trafford, Moyes alipewa kazi ya umeneja katika klabu ya Real Sociedad ya Uhispania lakini akafutwa kazi Novemba mwaka huu baada ya klabu hiyo kutofanya vyema.