Arsenal kukabiliana na Newcastle

Arsenal Haki miliki ya picha Getty
Image caption Arsenal wanaongoza kwenye jedwali la ligi

Klabu nyingi za Ligi Kuu ya England zitashuka dimbani Jumamosi kusaka alama za kwanza Mwaka Mpya, Arsenal wakijaribu kuendeleza uongozi kileleni kwa mechi ya nyumbani dhidi ya Newcastle.

Manchester United nao watakuwa nyumbani Old Trafford kusakata gozi dhidi ya Swansea ambao kwenye mechi za hivi karibuni wamekuwa wakiwalemea.

Manchester City watakuwa ugenini baadaye dhidi ya Watford.

Chelsea watasubiri hadi Jumapili kujaribu bahati watakapokuwa ugenini dhidi ya Crystal Palace.

Ratiba kamili ya mechi ni kama ifuatavyo:

Jumamosi 2 Januari 2016 (Saa za Afrika Mashariki)

 • West Ham v Liverpool 15:45
 • Arsenal v Newcastle 18:00
 • Leicester v Bournemouth 18:00
 • Man Utd v Swansea 18:00
 • Norwich v Southampton 18:00
 • Sunderland v Aston Villa 18:00
 • West Brom v Stoke 18:00
 • Watford v Man City 20:30

Jumapili 2 Januari 2016

 • Crystal Palace v Chelsea 16:30
 • Everton v Tottenham 19:00

Jumanne 2 Januari 2016

 • Aston Villa v Crystal Palace 22:45
 • Bournemouth v West Ham 22:45
Haki miliki ya picha Getty
Image caption Swansea walikuwa klabu ya kwanza kushinda mechi dhidi ya Man Utd chini ya Louis van Gaal AGosti 2014