Beki wa zamani wa Wigan afariki

Gohouri Haki miliki ya picha Getty
Image caption Gohouri alitoweka tarehe 12 Desemba mwaka jana

Beki wa zamani wa Wigan Athletic Steve Gohouri amefariki akiwa na umri wa miaka 34.

Gohouri alichezea Wigan mechi 42 kati ya 2010 na 2012 na alichezea timu ya taifa ya Ivory Coast mechi 12.

Gohouri aliripotiwa kutoweka tarehe 12 Desemba baada ya kuhudhuria sherehe ya Krismasi ya klabu yake ya TSV Steinbach ya Ujerumani. Alikuwa amepanga kutembelea familia yake Paris lakini hakufika.

Polisi wa Ujerumani wamethibitisha mwili wa mchezaji huyo umepatikana ndani ya Mto Rhine katika jiji la Krefeld, magharibi mwa nchi hiyo.

Taarifa ya polisi imesema hakuna dalili zozote kwamba Gohouri aliuawa.

Wigan Athletic wameandika kwenye Twitter: "Tunahuzunishwa na habari za kifo cha difenda wetu wa zamani Steve Gohouri. Tunaomboleza na familia.”

Gohouri alihamia Ufaransa kutoka Ivory Coast akiwa na umri wa miaka mitano, na alilelewa viungani mwa mji wa Paris.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Gohouri amekuwa akichezea TSV Steinbach

Alianza uchezaji wake Ufaransa lakini pia alichezea klabu za

Israel, Uswizi, Liechtenstein, Ugiriki na Ujerumani.

Alijiunga na Wigan, kutoka Borussia Monchengladbach ya Ujerumani, Januari 2010, klabu hiyo ilipokuwa bado inacheza Ligi Kuu ya England.