Yanga yatoa dozi Kombe la Mapinduzi

Michuano ya kombe la mapinduzi 2016 imeanza mwanzoni mwa wiki hii, visiwani Zanzibar kwa mechi mbili za kundi B, katika mchezo wa awali Timu ya Mafunzo ikicheza na Yanga ilipoteza mchezo huo kwa kipigo cha mabao 3-0, mabao ya Yanga yalifungwa na wachezaji Dolnad Ngoma mabao 2, na Paul Nonga akifunga bao 1.

Katika mchezo wa pili Mtibwa Sugar ikicheza na Azam FC mchezo huo ulimalizika kwa sare ya bao 1-1.

Michuano hiyo inaendelea tena hii leo Jumatatu kwa michezo miwili ambapo JKU ya Zanzibar itamenyana na URA ya Uganda, na Simba itachuana na Jamhuri .