Stoke kuikabili Liverpool Capital One

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Stoke City walipokuwa wakimenyana na Swansea

Mechi za kwanza za nusu fainali ya Capital One Cup, ambalo ni Kombe la Ligi huko England, zitachezwa leo Jumanne Usiku Januari 5 na Jumatano Januari 6.

Leo Jumanne Stoke City watakuwa nyumbani Britannia kuwakaribisha Liverpool na kesho Jumatano Everton watakuwa Goodison Park na Man City.

Nusu Fainali za michuano hiyo zitachezwa kwa mikondo miwili ya nyumbani na ugenini na timu zitarudiana tena hapo Januari 26 na 27.

Timu ambazo zimetinga hatua ya nusu fainali ni Stoke baada ya kuibwaga Sheffield Wednesday na Liverpool kuitoa Southampton wakati Everton waliwatoa Middlesbrough na Man City wakiitupa nje Hull City.

Bingwa Mtetezi wa Kombe hili alikuwa Chelsea ambae alitupwa nje na Stoke City kwa Mikwaju ya Penati 5-4 baada ya Sare ya 1-1.