Fifa yataka Valcke apigwe marufuku miaka tisa

Valcke Haki miliki ya picha Getty
Image caption Valcke tayari alikuwa awali amepigwa marufuku ya kutojihusisha na soka kwa siku 90

Kamati ya maadili ya FIFA imependekeza katibu mkuu wa shirikisho hilo linalosimamia soka duniani Bw Jerome Valcke apigwe marufuku miaka tisa.

Anadaiwa kutumia vibaya pesa pamoja na kukiuka sheria nyingine za Fifa.

Kamati hiyo imependekeza Valcke azuiwe kushiriki shughuli zozote za michezo kwa siku nyingine 45, juu ya marufuku ya siku 90 ambayo ameitumikia, kusubiri uamuzi kuhusu marufuku ya miaka tisa waliyoipendekeza.