Liverpool yaichapa Stoke Capital One

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Jordon Ibe

Klabu ya soka ya Liverpool hapo jana ilifanikiwa kuifunga Stoke City bao 1-0 katika mchezo wa kwanza wa hatua ya nusu fainali ya michuano ya Capital One katika mchezo uliopigwa dimba la Brittania.

Bao pekee la Liverpool lilifungwa na mchezaji Jordon Ibe katika dakika ya 37 kipindi cha kwanza ushindi ambao umempa furaha kocha Jurgen Klopp na kumpa matumaini ya kutinga fainali ya michuano hiyo.

Iwapo watafanikiwa mechi ya marudiano, Liverpool watakutana na mshindi wa nusufainali kati ya Everton au Manchester City, kwenye fainali ambayo itachezewa uwanja wa Wembley.

Mechi ya kwanza ya nusufainali hiyo nyingine itapigwa usiku wa leo ambapo Everton watakuwa nyumbani Goodson Park dhidi ya Manchester City.