Samatta Nigeria sherehe za kutuza wachezaji

Image caption Mbwana Samatta

Mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Tanzania na klabu ya TP Mazembe ya Congo DR, Mbwana Samatta leo hii anatarajiwa kuwasili nchini Nigeria kuhudhuria sherehe za utoaji wa tuzo kwa wachezaji bora barani Afrika zitakazofanyika katika mji wa Abuja Alhamisi tarehe 7 Januari.

Mbwana Samatta anawania tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kwa wachezaji wa ndani, huku pia akiwa mfungaji bora wa michuano ya Ligi ya Mabingwa (CAF CL) baada ya kuifungia klabu yake ya TP Mazembe mabao 8 na kuibuka mabingwa wapya wa michuano hiyo.

Samatta anawania tuzo ya mchezaji bora wa Afrika pamoja na mlinda mlango wa TP Mazembe, Robert Kidiaba (Congo DR) na mshambuliaji wa Etoile du Sahel Baghdad Boundjah (Algeria).

Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Mwesigwa Selestine ameandamana na Samatta kuhudhuria sherehe hizo.