Januzaj kurejea Manchester United

Man Utd Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Manchester United wanasema hajachezeshwa vya kutosha Borussia Dortmund

Manchester United imemwita nyumbani Adnan Januzaj kutoka Borussia Dortmund ambako amekuwa kwa mkopo wa msimu mmoja.

United wamemtaka mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ubelgiji arejee Old Trafford kwa sababu ya kukosa kuchezeshwa Ujerumani.

Januzaj, mwenye umri wa miaka 20, amecheza mechi 12 pekee katika klabu hiyo ya Bundesliga, sana akiingia kama nguvu mpya.

Ni mara tatu pekee ambapo alikuwa kwenye kikosi cha kuanza mechi.

Mechi zote alizochezeshwa ligini, ambazo ni mechi sita, aliingia kama nguvu mpya.

Hajachezeshwa hata mara moja tangu mechi ya Europa League ambayo walichapwa na PAOK Salonika tarehe 10 Desemba.

Januzaj alichezea United mechi nne Agosti na ndiye aliyewafungia bao la ushindi ugenini Aston Villa mwezi huo.

Haki miliki ya picha PA

Mkataba wake Old Trafford utamalizika 2018.