Ugaidi:Sheria kubadilishwa Ujerumani

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Merkel

Chansela, wa Ujerumani Angela Merkel,amesema kuwa serikali lazima iangalie suala la mabadiliko ya sheria, baada ya wimbi la mashambulio dhidi ya mwanamke katika mji wa Cologne wakati wa sherehe za mwaka mpya.

Bi Merkel amesema kuwa ni muhimu kuwa wazi kwa ukamilifu na namna ya kushughulikia suala hilo.

Wajerumani wameshtushwa na matukio ambapo mwanamke mmoja alitekwa, kuporwa na kunyanyaswa kingono, na kundi la wanaume ambao walioshuhudia tukio hilo wanasema walionekana kutoka mataifa ya magharibi mwa Afrika ama waarabu .

Kumi na wanane kati ya washukiwa waliokamatwa walikuwa ni watu wanaoomba hifadhi ya ukimbizi .

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Wahamiaji

Mamia ya watu wanatazamiwa kushiriki maandamano katika mji wa cologne leo yaliyoandaliwa na vugu vugu la mrengo wa kulia la Pegida .

Mashambulio hayo yamezua mjadala mkali kuhusu sera ya Ujerumani ya kuwafungulia milango wahamiaji.

Mwaka jana Ujerumani iliwakaribisha wahamiaji takriban milioni moja.