Liverpool yanusirika FA

Haki miliki ya picha AP
Image caption Liverpool ikicheza na Exeter

Kilabu ya Liverpool nchini Uingereza imenusurika baada ya kulazimisha droo ya 2-2 dhidi ya kilabu ya daraja la pili Exeter katika kombe la FA.

Liverpool ilitoka nyuma na kufanya mambo kuwa 2-2 na hivyobasi kulazimisha mechi ya marudiano ya raundi ya tatu.

Mkufunzi wa Liverpool Jurgen Klopp alifanya mabadiliko 11 na hivyobasi kikosi chake kuwa nyuma mapema wakati Tom Nichols alipofunga.

Jerome Sinclair alisawazisha lakini wenyeji walioongoza tena wakati kipa Adam Bodgan alipofungwa kutokana na kona iliopigwa na Lee Holmes.

Huku mda ukiyoyoma,Brad Smith aliiokoa Liverpool kwa bao lilofungwa kwa uzuri mwingi.

Marudiano hayo yatakachozwa Anfield yanatarajiwa kuipatia Exeter pauni 700,000.