Messi awika Barcelona

Haki miliki ya picha epa
Image caption Washambuliaji wa Barcelona wakiongozwa na Lionel Messi

Lionel Messi alifunga mabao matatu na kuiwezesha Barcelona kupata ushindi wa rahisi dhidi ya Granada na kurudi kileleni mwa ligi ya La Liga.

Raia huyo wa Argentina alifunga mara mbili katika dakika 15 za kwanza na kuongeza bao jingine baada ya mda wa mapumziko hivyobasi kuongeza idadi ya mabao aliyofunga kufikia 18 huku Barcelona ikifaulu kucheza mechi 20 bila kupoteza.

Messi aliiweka Barcelona kifua mbele baada ya kupata pasi nzuri kutoka kwa mshambuliaji matata wa timu hiyo Louis Suarez.

Aliongeza bao la pili katika dakika ya 58 kabla ya Neimar kufunga bao la nne.