Arsenal,Man City na Man United zafuzu FA

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Sergio Aguero

Mabingwa watetezi wa Kombe la FA Arsenal walitoka nyuma na kuweza kufuza kwa raundi ya tatu ya kombe hilo baada ya kuicharaza Sunderland mabao 3-1.

Sunderland ilichukua uongozi wa ghafla wakati Jeremain Lens alipofinga akiwa nadni ya boksi baada ya beki Laurent Koscielny kufanya masihara.

Hatahivyo Arsenal ilisawazisha kupitia Joel Campbel na baadaye kuchukua uongozi kupitia bao la gusa ni guse lililofungwa na Aaron Ramsey.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Aaron Ramsey wa Arsenal akifunga

Baadaye mshambuliaji wa Arsenal Olivier Giroud alifanya mambo kuwa 3-1.

Kwengineko Sergio Aguero aliiongoza Manchester City kupata ushindi dhidi ya Norwich City.

Aguero aliwachenga mabeki wa Norwich na kuiweka kifua mbele City.

Haki miliki ya picha PA
Image caption Wayne Rooney

Baadaye Mshambuliaji huyo aliwachenga tena mabeki wa kilabu hiyo na kutoa pasi murua kwa mshambuliaji wa Nigeria Kelechi Iheanacho aliyecheka na wavu.

City ilitawala mchezo na haikuchukua mda mrefu Kevin De Bruyne alipofunga bao la tatu.

Nayo Mkufunzi wa kilabu ya Manchester United alioongoza timu yake kupata ushindi wa 1-0 dhidi ya Sheffiled United,bao lililofungwa kwa njia ya penalti na nahodha Wayne Rooney baada ya Memphis Depay kuangushwa katika eneo la hatari.

United ilishindwa kufunga kwa kipindi cha kwanza kwa mechi 11 ilizocheza na walibahatika walipopata bao hilo kunako dakika za lala salama.