Van Gaal:Baadhi ya mechi za United zinachosha

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Louis Van Gaal

Mkufunzi wa kilabu ya Manchester United Louis Van Gaal amesema kuwa amechoshwa na baadhi ya mechi za timu yake msimu huu.

''Kuna mechi ambazo hata mie nimezifurahia'',alisema raia huyo wa Uholanzi.Na pia kuna mechi ambazo zinachosha na kunikasirisha kwa sababu tunashindwa kupita safu ya nyuma ya upinzani ,lakini hiyo ni soka''.

Timu hiyo ya Van Gaal ilizomwa wakati wa mapumziko katika mechi ya kombe la FA siku ya jumamosi ambapo timu hiyo iliishinda Shiffield United 1-0,huku maelfu ya wafuasi wakiondoka mapema uwanjani.

Akiulizwa ni kwa nini mashabiki wengi waliondoka mapema kabla ya Wayne Rooney kufunga kupitia mkwaju wa penalti,kunako dakika ya 93,Van Gaal alijibu,''Hawafikirii kwamba tutafunga na pengine ni kwa sababu mashabiki ni wengi mno''.